MAOMBI NI ZAIDI YA KUOMBA ~ 3

Na Peter Mbelembe
3.Tambua nafasi ya neema na jenga tabia ya kuomba neema juu yako juu ya mambo uyaombeayo. Maana ya neema ni ule upendeleo wa pekee aupatao mwanadamu kwa Mungu wa kufanikishwa mambo yake hata kama hakustahili kisheria.mfano  Mariamu mamaye Yesu Kristo alipata neema ya kuwa mama wa mwokozi wa ulimwengu si kwasababu alikuwa bikira pekee Israel hapana, kwani kulingana na tamaduni za kiyahudi ilikiwa binti yeyote akikamatwa uasherati au ni mjamzito kabla ya kuolewa sharti auwe kwa kupigwa mawe hivyo mabinti wengi kwa kuogopa kifo ni lazima walijitunza na kuwa mabikira.Hivyo ni nini basi kilimfanya achaguliwe kuwa mama ni neema tu. Luk 1:28" Akaingia nyumbani kwake akasema, Salamu, uliyepewa neema, Bwana yu pamoja nawe." hiyo n salamu ya malaika ikisema ULIYEPEWA NEEMA.

Neema hiyo hutofautiana kati ya mtu na mtu vile mtu aiombavyo na Mungu atoaye apendavyo. Mfano kulikuwa na mitume 12 wa Yesu aliokuwa nao muda akiwa hai duniani lakini Petro pekee alikuja kuwa na upako mkuu sana zaidi ya wengine ila Paulo akawa nao zaidi ya wote japo hakulelewa na Yesu physically ila kiwango chake cha neema kilikuwa kikubwa.Tazama 1Kor 3:10" Kwa kadiri ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi, kama mkuu wa wajenzi mwenye hekima, naliuweka msingi, na mtu mwingine anajenga juu yake. Lakini kila mtu na aangalie jinsi anavyojenga juu yake." Anasema KWA KADIRI YA NEEMA YA MUNGU ALIYOPEWA yaani level tofauti na wengine kawa mjenzi mwenye hekima na kumbe yeye alipewa na huwezi pewa kama hauombi.
Hvyo bc nawe mpendwa jenga tabia ya kuomba na kuamini kuwa neema y Mungu pekee yaweza kusababisha upenyo kwko haijalishi hilo jmbo lilishawah ombewa na nani, anajina kubwa kiasi gn, au linamuda gn, Mungu yuko kazini kupitia wewe na neema yake yaweza kukufanya uvuke c kw sababu unakiroho kikubwa hapana.Ngoja nikujenge kidgo, "kunawakat nilikuwa kihuduma kijijin alikulelewa mzee wangu bc wakat wa maombi akaja mma mmoja aliyekuwa n tatizo la moyo wake kuzungukwa n maji mengi n miguu ilikuwa inawaka moto hvyo alikuwa hawez fanya kazi yyote ngumu kw miaka 7 na alikuwa mwalimu n ilikuwa wanafunz wakimkwaza kidgo anapoteza fahamu n anandgu zake wenye uwezo kiuchumi hvyo walimpeleka kila aina y hospitali na kila nyumba y maomb walivyoweza ila tatizo likabk palepale, alipokuja tumwombee nikamuulza historia yke kidgo akanieleza mambo mengi sna n hadi majina ya watumish wengne ambao kwngu n baba zangu kihuduma akayataja kw kweli ndn yngu nilijickia kutokuwa n haki ya kumwombea kma ashapita huko kote lkn neno lilikuja juu yngu kuwa iko neema y uponyaji wake leo kupitia maombi hayo na nikatii na kumwombea na historia yke ikabadilishwa na Yesu mwenyewe cku ile."
Hata kwko ukiitambua nafasi y neema na ukaiheshimu na kuikiri yote uliyohc hayajibiwi yanijibiwa ktk jina la Yesu.Inuka anza tena kuliombea hilo jmbo mpka kieleweke. 1 2 3 4 5

0 comments:

Post a Comment