Yaani hapa si suala la kukaa usiku mzima bila kulala na ukasema nimekesha yaweza kuwa kweli kwa baadhi ya watu ila kwa wengine ikawa ni uongo LAKINI KUKESHA HASA KUNAKOZUNGUMZIWA NI KULIOMBEA JAMBO BILA KUNYAMAZA HADI UONE MAJIBU HAIJALISHI NI KWA MUDA GANI.Tazama Mark 14:37" Akaja akawakuta wamelala usingizi, akamwambia Petro, Je! Simoni, umelala? Hukuweza kukesha saa moja? 38 Kesheni mwombe, msije mkaingia majaribuni, roho i radhi ila mwili ni dhaifu. 39 Akaenda zake tena, akaomba, akisema neno lilo hilo."
Unaona hapo juu Yesu anawaambia hawakuweza kukesha naye hta saa 1 yaani kuiombea safari yake Yesu ya mateso mpaka Yesu aone upenyo wa kuukabili msalaba na baada ya kuwaambia akarudi tena kuomba akiliombea jambo lilelile tena.kwenye biblia ya kiingereza mstari wa 14:38" Keep awake and watch and pray [constantly], that you may not enter into temptation; the spirit indeed is willing, but the flesh is weak."(AMP). Note: 'pray constantly'.
Ndugu waweza kuomba vizuri kabisa na hunatamaa binafsi ya kutaka kujitwalia utukufu wa Mungu ila si kila kitu utakachoomba kitajibiwa muda huohuo hata kama ndio umeahidiwa muda huohuo na Roho Mtakatifu kunabaadhi ya mambo unahitaji uyasukume kwa maombi kwa nguvu iwe kwa kufunga na kuomba au kukaa ukiliombea bila hata kufunga mpaka limetokea ndipo unanyamaza kimya na si kila ukiomba na kaupako kakakata na huoni majibu unakimbilia tu kuwa ""aaahh baba mapeniz yako yatimilike tu" "hakuna cha mapenzi hapo kesha mpaka kieleweke na hiyo ndiyo siri kubwa ya wababe wote kimaombi duniani.
Tumtazame siri iliyompa ushindi Eliya Mtishibi na kukesha kwenye kila alilokuwa analiombea Yakobo 5:17" Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinyeshe, na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita." SIKIA anasema akaomba kwa BIDII. Sasa wewe ndugu yangu umeomba kidgo tu hujaona upenyo unaanza kulaumuuu au umeridhiika kama umepeleka maombi yako dampo hivyo kuwa hakuna majibu zaidi ya uvundo, Mungu wetu hayuko hivyo anza kukesha leo juu ya kila jambo na omba vizuri mpaka kieleweke na hujachelewa inuka sasa katika jina la Yesu!!
1 2 3 4 5
0 comments:
Post a Comment