MAOMBI NI ZAIDI YA KUOMBA-1

Na Peter Mbelembe
Neno MAOMBI ni neno maarufu sana maeneo mengi na kwa watu wengi hasa baadhi wakiwa wanapitia magumu au wengine kwa hiyari yao tu wakifanya mawasiliano na Mungu wetu aliyepo ila haonekani kwa macho ya nyama ili asababishe mabadiliko fulani juu ya jambo hilo liombewalo. Na husisitizwa na wanadamu hata Mungu mwenyewe tazam Isaya 43:26" Unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako." Kumbe unahaki zako rohoni ila huwezi zipata bila kujieleza kwake Mungu.

Lakini cha ajabu kunabaadhi ya watu wamekuwa wakiomba au kuombewa sana kwa muda mrefu na hata ikabidi wabadili staili mbalimbali za maombi kma kufunga, kukesha, kuweka nadhiri, kutoa sadaka za kupanda mbegu,kuomba kwa kulia,wengne sauti ndogo,kubwa na ikibidi hata kunena kwa lugha japo hata kama hawana hiyo karama lakini bado hayaonekani mabadiliko yoyote jambo linalosababisha wengi kubaki njia panda.Mfano wengine kutokana na kutoona majibu wameamua kumwacha Mungu kabsa, wengine wamezira kuomba ila wanajifarji kuwa bado wanampenda Mungu,wengine wamefuta namba za simu za watumishi waliokuwa wanashirikiana nao kuomba kisa eti pengine hawana upako wa kutosha ndio maana hakuna majibu,wengine wakijipa moyo kuwa Mungu amesema nisubiri japo hakuna hata chembe la sauti ya huyo Mungu, wengine wameamua kupita njia za mkato juu ya walilokuwa wakiliombea ikibidi hata kwa rushwa iwe ya pesa hata miili na baadae wanakuja kushuhudia madhabahuni etii Bwana ametenda ila ukweli unaujua mwenyewe.
Lakini kwanini hayo yote yatokee wakati Mungu anatuhimiza tuombe? Kunakitu muhimu lazima tutambue kuwa maombi si ishu ya kuomba tu kunavigezo na masharti muhimu ya kuzingatia na ukiyakataa maarifa haya lazima uangmie eneo la maombi.Yafuatayo ni mambo muhimu:-
 🔻Jitahid kuomba vizuri.
Tazama Yakobo 4:3" Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu."yaani lolote uombewalo au uombalo hakikisha ni kile ambacho Mungu anatamani kitokee na Yeye kupewa sifa na utukufu na sio wewe kupewa sifa na utukufu.Mfano kuna siku nilikuwa nimeingia kwenye daladala na ninaharaka na nimekuta abiria wawili tu, kwa kujiona mimi wa kiroho sana nikaanza kuulazimisha ulimwengu. wa roho umshurutishe derva aondoe gari japo tuko wachache nikijisahaulisha kuwa yeye yuko kazini na ni mpango wa Mungu afanye kazi hyo na Mungu ainuliwe kwa mapato yake huyo dereva, ila mimi nakusudia kumtia hasara na nilisimamia andiko la 2Kor 10:3" Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; 4 (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;) 5 tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;" ona hapo TUKIANGUSHA KILA MAWAZO na mimi nikawa naangusha mawazo ya dereva ili aondoe gari kwa hasara. unadhani Mungu alifanya huo uzembe niliokuwa naomba? na unadhani nilijisikiaje moyoni, niliona kiroho changu kimepoa?!!
Vivyo hvyo jitahidi sana kujua ipi ni tamaa ya Mungu juu ya hilo uliombealo na i kile ujisikiacho wewe kwani hata kama utatoaje machozi Mungu anauchungza moyo Tazama Yer 17:9" Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua? 10 Mimi, BWANA, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake.".Bwana anauchungza moyo.
Omba leo vitu uvitamanivyo na Mungu anavitamani na mwisho wa siku sifa na utukufu jipange kumrudishia Mungu uone Bwana anavyojifunua katika jina la Yesu.

1 2 3 4 5

0 comments:

Post a Comment